IQNA

Mabango ya kampeni ya kuunga mkono Hijabu Chicago, Marekani

12:00 - February 17, 2018
Habari ID: 3471395
TEHRAN-(IQNA)-Kundi la Kiislamu la GainPeace lenye makao yake katika mji wa Chicago nchini Marekani limezindua kampeni ya mabango yenye kuunga mkono hijabu kama vazi lenye kumpa uwezo mwanamke.

TEHRAN-(IQNA)-Kundi la Kiislamu la GainPeace lenye makao yake katika mji wa Chicago nchini Marekani limezindua kampeni ya mabango yenye kuunga mkono hijabu kama vazi lenye kumpa uwezo mwanamke.

Kampeni hiyo ya wiki sita pia inalenga kuondoa  kuondoa dhana potovu kuhusu vazi hilo na pia kufafanua kuhusu namna mwanamke anavyoheshimiwa katika Uislamu.

Halikadhalika kamepni hiyo inakusudia kuwapa Wamarekani fursa ya kuitazama Hijabu kama vazi ambalo linampa mwanamke Mwislamu uwezo, nguvu na uhuru kinyume na inavyodaiwa kuwa vazi hilo linamdhulumu.

Mabango hayo yanaonyesha vazi la staha la Maryam SA, mama yake Nabii Issa-Yesu (AS) ambaye vazi lake lilishabiohiana na Hijabu ya sasa ya Waislamu huku ikisisitizwa kuwa vazi hilo linatizamwa kama vali la heshima na Wakristo na Waislamu duniani.

Kampeni hiyo pia kwa ujumla inalenga kuelimisha jamii ya Wamarekani kuhusu Uislamu ili kukabiliana na chuki dhidi ya dini hii tukufu katika vyombo vya habari nchini humo.

“Hijabu iko katika habari ima kwa mtazamo hasi au mtazamo chanya,” amesema Dkt. Sabeel Ahmad mkurugenzi wa mradi wa GainPeace. “Kampeni hii ya Hijabu inalenga kuelimisha jamii kuwa Hijabu ni nembo ya nguvu na vi vazi la kumdhalilisha mwanamke.”

3465211

captcha