Sherehe hiyo ilianza kwa mlango wa al-Kaaba kufunikwa kwa pazia hiyo ambalo baadhi ya sehemu zake zimenakishiwa kwa uzi wa dhahabu. Sehemu nne za pazia hilo zimepambwa kwa Surat al Ikhlas na aya nyinginezo za Qur'ani Tukufu.
Kila mwaka pazia la hariri ambalo huwa limefunika al-Kaaba hubadilishwa na jipya kuwekwa katika siku ya 9 ya Dhul Hija.
Pazia ambalo hutolewa hukatwa vipande vipande na kuzawadiwa wageni maalumu kutoka nchi za kigeni.