IQNA

Rais Iran katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Uturuki

Kadhia ya Palestina ni kadhia muhimu zaidi kwa umma wa Kiislamu

20:31 - May 16, 2021
Habari ID: 3473917
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na mwenzake wa Uturuki na kusisitiza kuwa kadhia ya Palestina ni kadhia muhimu zaidi ya pamoja kwa umma wa Kiislamu hivi sasa.

Katika mazungumzo hayo ya simu Jumapili, Rais Hassan Rouhani wa Iran amemfahamisha Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki kuwa kuna haja ya kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na kuhakikisha kuwa utawala huo unasitisha mara moja jinai za kinyama na mauaji ya Wapalestina madhulumu na wasio na ulinzi.

Rouhani amesema nchi za Kiislamu hasa Iran na Uturuki zinapaswa kutumia uwezo wao wote hasa uwezo wao katika taasisi za kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kukabiliana na jinai na uvamizi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Aidha rais wa Iran amesisitiza kuhusu umuhimu wa Iran na Uturiki kuwa na misimamo ya pamoja kwa ajili ya kukabiliana na migogoro ya kieneo ikiwemo migogoro ya sasa Syria na Yemen.

Kwa upande wake, Rais Erdogan wa Uturuki inasikitisha kuona jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina. Amesema jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua imara za kuzuia ujuma hizo na pia kuna haja ya kuwepo msimamo wa pamoja baina ya nchi za Kiislamu kuhusiana na kadhia ya Palestina.

3971914

captcha