IQNA

Watu wenye silaha wawateka nyara wanafunzi wa shule ya Kiislamu Nigeria

16:33 - May 31, 2021
Habari ID: 3473964
TEHRAN (IQNA)- Watoto wa shule moja ya Kiislamu wametkewa nyara na watu wasuojulikana ambao walishambulia shule yao katikati mwa Nigeria.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa polisi Wasiu Abiodun, wanafunzi karibu 200 wa shule ya Kiislamu ya Salihu Tanko eneo la Rafi katika jimbo Niger walitekwa nyara na watu ambao walikuwa wakifyatua risasi kiholela.

Msemaji wa polisi ameongeza washambuliaji waliwasili eneo la shule kwa pikipiki na kuanza kufyetua hovyo risasi zilizosababisha kifo cha mkaazi mmoja na kumjeruhi mwingine.

Hayo yanajiri siku moja baada ya msemaji wa polisi katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria kutangaza kuwa wanafunzi 14 waliokuwa wamesalia ambao walitekwa nyara katika Chuo Kikuu kimoja huko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo wameachiliwa huru. Tukio hilo limejiri ikiwa zimepita siku 41 tangu watekwe nyara na genge la wahalifu.

Matukio ya utekaji nyara yamekuwa yakifanywa mara kwa mara na magenge ya wahalifu nchini Nigeria ili kujipatia fedha huku kukiripotiwa matukio  ya utekaji nyara zaidi ya 730 0 tangu mwezi Disemba mwaka jana hadi sasa. Wananchi wa Nigeria wamekuwa wakifanya maandamano wakiwalaumu askari usalama na serikali kwa kushindwa kuyasaka magenge hayo ya utekaji nyara. 

Aprili 20 mwaka huu watu waliokuwa na silaha walivamia Chuo Kikuu cha Greenfield katika jimbo la Kaduna na kuwateka nyara wanafunzi wasiopungua 20 na kumuuwa mfanyakazi mmoja wa chuo hicho. Wanafunzi watano walinusuriwa kutoka mikononi mwa wahalifu hao siku chache baada ya tukio hilo baada ya familia na serikali kulazimishwa kutoa kikomboleo. 

3974699

Kishikizo: nigeria shule watoto
captcha