IQNA

Saudia yatetea uamuzi wa kupunguza sauti ya adhana nchini humo

17:31 - June 01, 2021
Habari ID: 3473969
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Masuala ya Kiislamu katika Ufalme wa Saudi Arabia ametetea amri yenye utata aliyoitoa ya kupunguza sauti katika adhana misikitini.

Abdul Latif Al Sheikh, Waziri wa Masuala ya Kiislamu amedai kuwa uamuzi wa kubana adhana umetokana na malalamikio kuhusu 'kiwango cha juu cha kelele'.

Kwa mujibu wa amri iliyotolewa na Abdul Latif Al Sheikh kwa misikiti yote katika ufalme huo, vipaza sauti vitatumika tu wakati wa adhana na iqama na pia sauti  inapaswa kuwa ya kiwango cha chini sana kuliko iliyvyo hivi sasa.

Amesema ametoa amri hiyo kwa kutegemea fatwa za wanazuoni maarufu Sheikh Mohammed bin Saleh Al Othaimeen and Saleh Al Fawzan ambao wanasema vipaza sauti vinapaswa kutumika tu wakati wa adhana na iqama.

Katika ujumbe ambao ametuma kwa njia ya video baada ya malalamiko makali kuibuka kufuatia amri yake, Al Sheikh amesema "wale wanaotaka kuswali hawahitaji kusubiri adhana bali wanapaswa kufika msikitini mapema."

Aidha amesema kwa kuzingaita kuwa televisheni za Saudia hurusha hewani adhana na sala, vipaza sauti misikitini havina matumizi makubwa.

Wasaudi wanaopinga amri hiyo wameanzisha kampeni katika mitandao ya kijamii na kusema kama sauti ya adhana inabanwa basi migahawa nayo inapaswa kuamurishwa kupiga marufuku miziki ambayo kawaida huwa inarushwa kwa sauti za juu kupita kiasi.

Al Sheikh amedai kuwa wanaopinga uamuzi huo wa kubana adhana ni  'maadui wa ufalme' na 'wanalenga kuchochea fikra za umma'.

Uamuzi huo wa kubana adhana misikitini Saudia unaonekana kuenda sambamba na mabadiliko ambayo yanaletwa na Mrithi wa Kiti cha Ufalme Mohammad bin Salman, ambaye anatakwa kuwa kiongozi asiye rasmi wa nchi. Bin Salman anatakaleza sera za kupunguza utambulisho wa kidini katika ufalme huo ambao kwa miongo kadhaa umekuwa ukitekeleza mafundisho ya pote la Kiwahhabi. Wahubiri wanaopinga sera hizo za Bin Salman wanakamatwa na kufungwa jela.

/3474864

captcha