IQNA

Kanali ya Kiswahili ya YouTube kuhusu fikra za Imam Khomeini (MA) yazinduliwa

20:15 - June 02, 2021
Habari ID: 3473973
TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania kimezindua Kanali ya YouTube kwa lugha ya Kiswahili kuhusu sira na fikra za Imam Khomeini-Mwenyezi Mungu Amrehemu, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu Iran (ICRO), kanali hiyo ya YouTube ina video zinazohusu maisha ya Imam Khomeini (MA) kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.

Kanali hiyo imezinduliwa kwa munasaba wa kumbukumbu yamwaka wa 32 tokea aage dunia Imam Khomeini (MA).

Taarifa hiyo aidha imesema semina kuhusu "Mtindo wa Maisha kwa Mtazamo wa Imam Khomeini (MA)" itarushwa moja kwa moja kupitia kanali hiyo ambayo anwani yake ni www.youtube.com/channel/UCsP3Ax93KJZ4IqCgrZKqvXw


3975031

captcha