IQNA

Misikiti yafunguliwa tena nchini Lebanon baada ya mwaka moja na nusu

23:31 - June 13, 2021
Habari ID: 3474003
TEHRAN (IQNA)- Misikiti imefunguliwa tena Lebanon baada ya kufungwa kwa muda mrefu kutokana na janga la COVID-19 au corona.

Kwa mujibu wa taarifa, hafla maalumu ya kufunguliwa tena misikiti nchini humo imefanyika mjini Baalbek kaskazini mashariki mwa Beirut katika Msikiti wa Imam Ali AS.

Hafla hiyo imeongozwa na Sheikh Tamr Hamza mkuu wa wahubiri wa Kiislamu na harakati za kiutamaduni katika eneo la Beqaa ambapo sasa misikiti ya Lebanon itafunguliwa lakini kwa kuzingatia mashrati maalumu ya kuzuia kuenea corona.

Misikiti ya Lebanon ilikuwa imefungwa kwa muda wa mwaka moja na nusu kutokana na hali mbaya ya maambukizi ya corona nchini humo. Sheikh Hamza amesema wasimamizi wa misikiti watakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa masharti ya kiafya yanazingatiwa.

3977245

Kishikizo: lebanon misikiti Corona
captcha