IQNA

Shughuli za Qur'ani

Vituo vya kusoma Qur’ani vimewekwa Najaf kabla ya 28 Safar

23:05 - September 23, 2022
Habari ID: 3475829
TEHRAN (IQNA) - Vituo vitano vya kusoma Qur'ani vimeanzishwa katika mji wa Najaf nchini Iraq huku waumini wakijitayarisha kushiriki katika maombolezo kwa mnasaba wa kukumbuka siku ya kuaga dunia Mtume Muhammad (SAW) katika siku zijazo.

Vituo hivyo vimewekwa kutoa huduma mbali mbali za Qur’ani kwa wafanyaziara ikijumuisha usomaji sahihi wa Qur’ani Tukufu hasa sura fupi fupi ambazo husomwa sana wakati wa Sala.

Vituo hivyo vinavyosimamiwa na kituo chenye uhusiano na Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Hazrat Abbas (AS), vitakuwa na wataalamu  zaidi ya 25 wa Qur'ani, wasomaji na waliohofadhi Qur’ani Tukufu.

Siku ya 28 ya mwezi wa mwandamo wa Safar ni kumbukumbu ya kuaga dunia Mtume Muhammad (SAW) na kuuawa shahidi Imam Hassan Mujtaba (AS), Imam wa pili wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia.

Maelfu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wanatarajiwa kuzuru kaburi tukufu la Imam Ali (AS) mjini Najaf kuadhimisha siku hiyo ambayo mwaka huu inasadifiana na Septemba 25.

3480593

captcha