IQNA

Fikra za Kiislamu

Riba hupelekea kuharibika mizani ya maisha

23:37 - September 23, 2022
Habari ID: 3475830
TEHRAN (IQNA) – Uislamu unasisitiza juu ya mwingiliano mzuri wa kiuchumi, ukisisitiza kwamba mtu anapaswa kujitahidi kupata pesa kwa nj ambazo ni ‘Halal’ au kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa Uislamu, wale wanaotaka kutumia riba kupata pesa bila ya kufanya juhudi zozote wanaharibu uwiano wa kiuchumi katika familia na jamii.

Riba ni faida isiyo halali mtu anapomkopesha mtu mwingine pesa na kutafuta faida zaidi.

Riba imetajwa na kulaaniwa katika aya kadhaa tofauti katika Quran Tukufu. Imeharamishwa katika Uislamu na kuzingatiwa kuwa ni dhambi kubwa inayoleta adhabu katika ulimwengu huu na ujao.

Aya ya 130 ya Surah Al Imran inasema: “Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa.”

Qur’an katika Aya nyingine inaelezea hatima ya wale wanaopokea Riba: “Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu." (Surah Al-Baqarah, Aya ya 275)

Kwa mujibu wa Quran, riba ni chanzo cha uharibifu na wale wanaokula riba husababisha madhara katika maisha ya familia na kijamii.

3480528

captcha