IQNA

Kushadidi chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya

16:17 - February 09, 2015
1
Habari ID: 2829282
Kuongezeka vitendo vya ukandamizaji dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa kumeendelea kulaaniwa na kukosolewa na jamii ya Waislamu sio tu nchini humo bali pia katika bara zima la Ulaya.

Radiamali ya Waislamu wa Ulaya kwa vitendo vya chuki dhidi ya dini yao Tukufu huko Ufaransa ni dhihirisho la kukerwa kwao na jinsi mizizi ya fitina na chuki dhidi ya Uislamu inavyozidi kusambaa kwa kasi katika bara hilo. Ni kutokana na hali hiyo, ndiyo maana Waislamu nchini Uingereza wakaandaa maandamano makubwa kulalamikia vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu ndani na nje ya Uingereza. Waandalizi wa maandamano hayo wamesema mara hii walikwenda mpaka ofisini kwa Waziri Mkuu, David Cameron kuwasilisha rasmi malalamiko yao.
Katika siku za hivi karibuni na tangu kutokea shambulizi dhidi ya ofisi za jarida la kila wiki la Cherlie Hebdo nchini Ufaransa mwanzoni mwa mwezi uliopita, ukandamizaji, udhalilishaji na chuki dhidi ya Uislamu vimeongezeka maradufu barani Ulaya. Jarida hilo mara kadhaa limekuwa likimvunjia heshima Mtume Mtukufu, Muhammad SAW kwa kumsawiri kupitia vibonzo. Licha ya Waislamu kukosoa na kulaani udhalilishaji huo, viongozi wa Ulaya wamekuwa wakisisitiza kuwa hawawezi kuingilia kadhia hiyo kwani jarida lenye kufurutu ada la Charlie Hebdo linatumia uhuru wake wa kujieleza. Baraza la kupambana na hofu na chuki dhidi ya Uislamu (Islamaphobia) nchini Ufaransa limesema tangu watu wenye silaha wavamie ofisi za Cherlie Hebdo Januari 7 mwaka huu, kumeshuhudiwa zaidi ya visa 50 vya uvamizi na ukandamizaji dhidi ya Waislamu.
Nchini Ujerumani nako, makundi yanayoeneza propaganda chafu na chuki dhidi ya Uislamu yamezidi kupata nguvu; na inavyoonekana, wimbi jipya la harakati hiyo linazidi kuibuka na kuenea kote barani Ulaya. Hata hivyo, kusimama kidete Waislamu wa Ulaya kumezuia kwa kiwango fulani, kasi ya kuenea harakati hizo. Baraza Kuu la Waislamu nchini Ujerumani linasema kuwa, wanawake Waislamu wenye kuvaa hijabu pamoja na mashekhe wenye kuva kofia na vilemba wamekuwa wakisumbuliwa na kunyanyaswa na makundi ya Wakristo yenye kufurutu ada katika miezi ya hivi karibuni. Baraza hilo pia limesema takriban kila wiki misikiti hushambuliwa ima kwa mawe au kwa mabomu ya petroli na vijana wa makundi yanayoeneza chuki dhidi ya Uislamu.
Ni mazingira kama hayo yanayowafanya Waislamu wa barani Ulaya kuingiwa na wasiwasi zaidi siku baada ya siku. Hii ni katika hali ambayo, serikali za nchi za Ulaya badala ya kulishughulikia tatizo la chuki na hofu dhidi ya Uislamu (Islamophobia) na kulipatia ufumbuzi, wamebaki kimya; na wanapozungumza wanatumia visingizio kama shambulizi dhidi ya jarida la Charlie Hebdo kuhalalisha uafiriti unaofanywa na raia wao dhidi ya jamii ya Waislamu.../mh

2826969

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Bila jina
0
0
Al islaam dini watakubali tu?
captcha