IQNA

Ripoti Maalumu ya IQNA

Kuenea chuki dhidi ya Ushia Afrika baada ya uvamizi wa Saudia Yemen

15:00 - June 18, 2015
Habari ID: 3315877
Sambamba na kuanza hujuma ya hujuma ya kijeshi ya Saudi Arabia nchini Yemen, kumeshuhudiwa kuongezeka kwa kasi chuki dhidi ya Ushia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran barani Afrika.

Ingawa kueneza chuki hizo ni katika kazi za kawaida na za daima za wahubiri wa Kiwahabi, lakini baada ya kuanza hujuma ya kinyama ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen tarehe 26 mwezi Machi, kumeshuhudiwa kuongezeka kwa kasi propaganda dhidi ya Ushia na Iran. Hivi sasa Mawahabi wanajipenyeza katika maeneo ya watu wasiojiweza na dhaifu barani  Afrika ambapo wanaeneza chuki dhidi ya Ushia na Iran kwa kutumia misikiti, shule, mikutano ya kijamii. Aidha katika kueneza upotofu wao, wanatumia mitandao ya kijamii katika intaneti, radio na televisheni.
Uchunguzi umebaini kuwa kila mara madola ya kiistikbari na kibeberu, kinara wao akiwa Marekani, yanapochukua hatua za kichokozi dhidi ya nchi za Waislamu, Mawahabi na taasisi zinazofungamna nao hupewa jukumu la kuhalalisha kidini ukatili wa mabeberu na waitifaki wao. Kiwango na wingi wa harakati za Mawahabi barani Afrika hufungamanishwa na maudhui zinazohusu chuki dhidi ya Ushia na Iran.
Kuanzia mwaka 2011 wakati wa mwamko wa Kiislamu katika nchi za Kiarabu za Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, mwamko ambao ulipata ilhamu kutoka Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Mawahabi walianzisha wimbi kubwa sana la propaganda dhidi ya Ushia na Iran lengo likiwa ni kupotosha mwamko wa Kiislamu katika umma.
Kwa mfano nchini Sierra Leone magharibi mwa Afrika kuna Radio au Idhaa ijulikanayo kama ‘Sauti ya Kiislamu’ ambayo inamilikiwa na Mawahabi nchini humo. Katika radio hiyo, wahubiri wa Kiwahabi magharibi mwa Afrika vinara wao wakiwa ni Ahmed Ramadhan Jalloh, Omar Farouq Bah na Ibrahim Bari wanaongoza propaganda dhidi ya Ushia na Iran. Tokea mwanzo wa hujuma ya kijeshi ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen, Mawahabi wameshadidisha propaganda zao hizo katika vyombo vya habari kwa kutegemea mihimili ifuatayo:
• Ushia unaenea kwa kasi, na eti ni hatari na inapaswa kupambana nao
• Eti Mashia wanakaribiana na Mayahudi na wana nukta zapamoja na Uyahudi!
• Eti Mashia wanawavunjia heshima masahaba na wakeze Mtume SAW.
• Eti Mashia wanapanga kubadilisha kibla cha Waislamu.
• Eti Mashia wanakusudia kuharibu mij mitakatifu ya Makka na Madina ili Karbala iwe kibla cha Waislamu na kwamba eti hatua hiyo inachukuliwa kufuatia agizo la Ahlul Bayt AS dhidi ya Ahlul Sunna.
Sambamba na hayo wahubiri wa Kiwahabi barani Afrika wanahalalisha na kutetea hujuma ya Saudia dhidi ya Yemen kwa kudai kuwa:
• Eti hujuma ya Saudia Yemen inalenga kuzima moto wa fitina na kuhifadhi umoja wa umma.
• Eti uamuzi wa Mfalme wa Saudia ni chanzo cha wokovu wa watu wa Yemen
• Eti hujuma ya kijeshi dhidi ya Yemen inalenga kudhamini usalama wa Makka na Madina.
• Mawahabi pia wanatakiwa kuomba dua kwa ajili ya ushindiwa jeshi vamizi la Saudia dhidi ya Yemen.
Radio ya ‘Sauti ya Kiislamu’ Sierra Leone imetoa wito kwa maimamu wa misikiti katika hotuba zao kuilaani Harakati ya Ansarullah nchini Yemen na kuunga mkono ukatili unaofanya na jeshi  Saudia nchini Yemen. Vibaraka na wanaohudumia Uwahabi barani Afrika wanawatuhumu Waislamu wa madhehebu ya Shia kuwa eti wanapanga njama dhidi ya Uislamu na Waislamu na kwamba wanapinga Sunna ya Mtume SAW sambamna na kuwasha moto wa vita katika nchi za Kiarabu. Pamoja na kuwa  utawala wa  kifalme Saudia unapata himaya kubwa kutoka nchi za Magharibi hasa Marekani na pia utawala haramu wa Israel, Wahubiri wa Kiwahabi wanahalalisha hujuma ya Saudia dhidi ya Yemen huku wakidai kuwa eti Mashia wanaunga mkono Wamagharibi na wanawahami Mayahudi. Katika wiki za hivi karibuni kumeshuhudiwa kuimarika kwa kasi harakati za wahubiri wa Kiwahabi barani Afrika. Misikiti na taasisi za Mawahabi katika nchi za kati na magharibi mwa Afrika kama vile Mali, Nigeria, Sierra Leone na Guinea zimegeuka na kuwa vitovu vya kueneza chuki dhidi ya Ushia.
Katika hali kama hii ni nini kifanyike? Katika hali kama hii ambapo Mawahabi wanatumia nembo za miji mitakatifu ya Makka na Madina  kuhalalisha jinai na upotofu wao miongoni mwa watu wanaodhulumiwa Afrika, ni nini kifanyike.?
Aghalabu ya vyombo vya habari barani Afrika havina uwezo wa kutosha wa kupata habari sahihi na hivyo katika  habari za kimataifa hutegemea vyombo vya habari vya Magharibi. Kwa hivyo kuna uwezekano wa kupotoshwa fikra za umma barani Afrika kutokana na propaganda  za Mawahabi dhidi ya Mashia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kukosekana majibu mafupi na marefu ili kuubainishia umma ukweli na kutofichuliwa njama za pamoja za madola ya Magharibi na Saudi Arabia ni nukta zinazowezea kupelekea waliowengi kuhadaiwa kuhusu Iran na Ushia.../mh

3315629

captcha