IQNA

Magaidi waua waumini 25 katika Msikiti Yemen wakati wa swala ya Idi

22:25 - September 24, 2015
Habari ID: 3367085
Waislamu 25 wa madhehebu ya Shia wameuawa shahidi na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a baada ya bomu kulipuka ndani ya msikiti wakati wa Swala ya Idul-Adh’ha mapema leo asubuhi.

Habari zaidi zinasema kuwa, watu wawili wanaoaminiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi na wakufurishaji la Daesh au ISIS ndio waliojiripua katikati ya Waislamu wakati wa Swala. Duru za hospitali zinasema kuwa, wengi wa majeruhi wako katika hali mbaya. Majengo yaliyo karibu na msikiti huo wa al-Balili yameharibiwa kabisa. Hadi tunakwenda hewani hakuna kundi lolote lilikuwa limedai kuhusika na mashambulizi hayo ya kinyama ingawa hujuma hiyo inafanana mno na mashambulizi ya huko nyuma ya Daesh au ISIS dhidi ya Mashia nchini Yemen.  Tayari viongozi mbalimbali wa Kiislamu wamelaani hujuma hiyo kwenye msikiti na katika siku tukufu ya Idul-Adh’ha.

3366952

captcha