Kwa mujibu
wa mwandishi wa IQNA, Hujjatul Islam Muhammad Ridha Hishmatu Mkuu wa Masuala ya
Qur'ani katika Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran, kama
ilivyokuwa katika miaka ya nyuma maonyesho hayo yatafanyika katika ukumbi huo
wa Sala. Amesema tayari mipango imeshaanza kufanikisha maonyesho hayo ambayo
hufanyika kila mwaka katika Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani. Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani huandaliwa na Wizara ya
Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran na kuleta pamoja mashirika na watu
wanaojihusisha na kazi zinazohusiana na Qur'ani Tukufu. Lengo kuu
la maonyesho ya Qur'ani katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni
kustawisha ufahamu wa Qur'ani na pia kueneza harakati za Qur'ani kitaifa na
kimataifa.