Mahathir Mohamad alikabidhi hati ya kujiuzulu kwake kwa mfalme wa Malaysia jana Jumapili.
Vilevile chama chake cha Parti Pribumi Bersatu Malaysia kimetangaza kwamba, kimejiondoa katika serikali ya mseto inayotawala Malaysia ya Alliance of Hope.
Uamuzi wa Mahathir unafuatia wiki ya malumbano ya kisiasa, baada ya kuripotiwa kwamba, chama chake kilikuwa kinapanga kuunda serikali mpya ambayo itamuweka kando mrithi wake mtarajiwa, Anwar Ibrahim.
Mzozo wa sasa kati ya wapinzani hao wawili wa muda mrefu yaani Mahathir, 94, na Anwar, 72, ni wa hivi karibuni zaidi katika mivutano ya muda mrefu ya kisiasa kati ya wanasiasa hao mashuhuri nchini Malaysia.