Siku ya Jumatatu, Idara ya Kitaifa ya Kukabiliana na Majanga UAE imesema hema hizo sasa zinapaswa kurejeshwa. Taarifa ya idara hiyo imesema uamuzi huo umechukuliwa kama sehemu ya stratijia ya kitaifa ya kudumisha afya ya umma na kurejesha hali ya kawaida katika maisha.
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu wa 1443 Hijria Qamaria unatazamiwa kuanza Aprili 2 2022 Miladia lakini kuanza huko kutategemea taarifa za mwezi mwandamo nchini UAE na maeneo mengine duniani.
Kabla ya janga la corona, hema hizo ambazo kwa kawaida huwa pembizoni mwa msikiti hutumika kuwalisha vibarua wenye kipato cha chini.