IQNA

Maumbile na Uislamu

Sala ya kupatwa kwa jua kusaliwa in UAE

16:59 - October 24, 2022
Habari ID: 3475984
TEHRAN (IQNA) – Misikiti katika nchi za Kiislamu huandaa sala maalum inayoitwa ' Salat Al-Ayat' wakati wa kupatwa kwa jua au mwezi, na kesho kutakuwa na kupatwa kwa jua

Kupatwa kwa jua kwa nadra kutapelekea kivuli cha mwezi kuonekana duniani Jumanne, Oktoba 25. Tukio hili la kipekee, ambalo lina mvuto wa aina yake na pia linaweza kuwashtua baadhi, ni ukumbusho kwa Waislamu kukumbuka uwezo wa Mwenyezi Mungu na kuwa waja watendao mema.

Katika Umoja wa Falme za Kiarabu na nchi nyingine za Kiislamu, sala ya Al-Ayat itaswaliwa kesho. Huko Dubai, sala itasaliwa baada ya Alasiri siku wakati kupatwa kwa jua kutakapoofikia kilele.

Ingawa si wajibu, sala hii ya kupatwa kwa jua inapendekezwa sana. Ni tofauti na sala za kila siku na kwa kawaida huswaliwa katika jamaa misikitini, ingawa pia familia zinaweza kuswali nyumbani pia.

Kupatwa kwa jua kwa sehemu ni tukio la nadra ambalo hutokea wakati mwezi unakuja kati ya jua na dunia. Kwa mujibu wa tovuti ya Khaleejtimes.com tukio hilo la anga linatarajiwa kuanza saa saan nane na dakika 42 na kumalizika saa kumi na dakika 54. Upeo wa kupatwa kwa jua utafanyika saa tisa na dakika 52 kwa saa za UAE.

3480983

Kishikizo: kupatwa kwa jua uae ayat
captcha