IQNA

Uhusiano wa nchi za Kiislamu

Shamkhani akiwa UAE: Ushirikiano na mshikamano vichuke nafasi ya mifarakano na uhasama

17:11 - March 17, 2023
Habari ID: 3476719
TEHRAN (IQNA)- Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesisitiza stratejia isiyobadilika ya sera za nje za Jamhuri ya Kiislamu kuhusu ushirikiano wa pande zote, endelevu na wenye manufaa na majirani zake na kusema: ili kuondokana na changamoto zilizopo ambazo kuendelea kwake hakuna maslahi kwa nchi yoyote katika eneo hili, ni lazima ushirikiano na mshikamano vichuke nafasi ya mifarakano na uhasama.

Admeri Ali Shamkhani mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na ambaye pia ni Katibu wa Baraza Kuu wa Usalama wa Taifa la Iran ametembelea Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE au Imarati) Alhamisi na amesema: Kuwepo hitilafu na hali ya kutoaminiana miongoni mwa nchi za eneo la kisratejia la Ghuba ya Uajemi ni kizuizi kikuu cha ustawi na uchumi wa eneo hilo na takwa la maadui wa nchi ajinabi. 

Afisa huyo wa ngazi ya juu wa usalama wa Iran ameashiria kuimarishwa uhusiano wa kisiasa na kiuchumi kati ya Iran na Imarati, na kusema kuwa nchi hizi mbili zinaweza kuchukua hatua kubwa katika kupanua ushirikiano wa pande zote na kuimarisha diplomasia ya ujirani.

Shamkhani aidha amesema matatizo ya eneo la Ghuba ya Uajemi yamechangiwa zaidi na uingiliaji wa nchi zilizo nje ya eneo hilo hususan Marekani na utawala wa Kizayuni na kuhimiza ulazima wa kuweko juhudi za pamoja za nchi za eneo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa eneo hili.

Rais wa UAE, kwa upande wake, alishukuru makubaliano ya hivi karibuni ya kihistoria ya kurejesha uhusiano kati ya Tehran na Riyadh ambayo alisema ni hatua madhubuti ya kusaidia zaidi kuleta maelewano kati ya nchi za kikanda.

Ameelezea matumaini yake kuwa ziara ya afisa mkuu wa usalama wa Iran huko Abu Dhabi itafungua ukurasa mpya katika uhusiano kati ya Iran na UAE.

Rais wa UAE alionyesha utayari wa nchi yake kutatua kutoelewana ili kukuza uhusiano wa pande mbili na Iran kwa kiwango cha juu.

Shamkhani pia amekutana  na Sheikh Tahnoun bin Zaid Al Nahyan Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati).

Katika kikao hicho Admeri Shamkhani amesema juhudi zinapaswa kufanyika ili kupanua na kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kiusalama, kiuchumi na kiutamaduni na kuzizuia nchi ajinabi kuchukua hatua zisizo na manufaa kwa kanda hii ya Ghuba ya Uajemi.   

Amesema, kubadilishana uwezo na tajiriba za kiuchumi, kibiashara na uwekezaji ni kati ya vipaumbele vikuu vya Jamhuri ya Kiislamu katika uhusiano wake na majirani zake na kwamba, kwa kuzingatia mazingira mazuri yaliyoandaliwa tangu mwaka mmoja uliopita kwa ajili ya kustawisha uhusiano kati ya Iran na Imarati, safari ya ujumbe wa Iran mjini Abu Dhabi ni mwanzo mwafaka kwa nchi hizo mbili kuingia katika awamu mpya ya uhusiano wa kisiasa, kiuchumi na kiusalama. 

Katika mazungumzo hayo, Sheikh Tahnoun bin Zaid Al Nahyan pia ameeleza kufurahishwa na ziara muhimu sana ya Admeri Ali Shamkhani katika Umoja wa Falme za Kiarabu na kusema kuwa, kushikiana na kuwa na urafiki na nchi kubwa na yenye nguvu ya Iran ni jambo muhimu na lenye thamani kubwa kwa Imarati.

Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Imarati amepongeza mapatano ya karibuni kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na utawala wa kifalme wa Saudi Arabia na kueleza kuwa, mapatano hayo yana jukumu kuu la kuimarisha amani, utulivu na usalama endelevu katika eneo la Magharibi mwa Asia. 

4128560

captcha