IQNA

Ukarimu katika Mwezi wa Ramadhani

UAE yazindua Kampeni ya 'Milo Bilioni 1' kwa wahitaji kote ulimwenguni

16:39 - March 27, 2023
Habari ID: 3476770
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zimezindua kampeni ya ukarimu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yenye lengo la kutoa msaada wa milo bilioni moja kwa wale wanaohitaji kote kote duniani.

Kampeni hiyo ya 'Milo Bilioni 1' iliyozinduliwa na Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, Makamu wa Rais wa UAE ambaye pia ni Waziri Mkuu na Mtawala wa Dubai, kwa lengo la kuzindua mfuko mkubwa wa msaada wa Mwezi wa Ramadhani, hadi sasa imepokea Dh247 milioni, wiki moja baada ya kuzinduliwa.

Kampeni hiyo hadi sasa imepokea michango kutoka kwa wachangiaji wakuu 13,220, watu binafsi, wafanyabiashara na wadau wa sekta ya umma na binafsi.

Mohammad Al Gergawi, Katibu Mkuu wa Taasisi ya 'Mohammed bin Rashid Al Maktoum Global Initiatives', alisema: "Kampeni ya 'Milo Bilioni 1' inaakisi maono ya Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum kwa kuendeleza juhudi za hisani, kufungua mlango kwa kila mtu ni onyesho la maadili yake ya muda mrefu ya kutoa na ukarimu, na uthibitisho wa hisia zake za kimaadili za kuwajibika kwa juhudi za kimataifa za kutokomeza njaa duniani kote."

Kampeni ya 'Ufadhili wa Milo Bilioni 1' inalenga kuunda suluhisho endelevu na kutekeleza mipango madhubuti ya kupambana na kutokomeza njaa, na kusaidia vikundi vilivyo katika hatari ya njaa kote ulimwenguni.

Kampeni ya 'Milo Bilioni 1' inafuatia mafanikio ya kampeni za awali za msaada wa chakula zilizozinduliwa chini ya maagizo ya Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum katika kipindi cha miaka 3 iliyopita, ambapo ya kwanza ilikuwa kampeni ya  Ramadhani ya 2020 ya "Milo Milioni 10", ambayo ilikuwaonyesho la kwanza na kubwa zaidi la mshikamano wa aina yake, kusaidia wahasiriwa wa janga la Covid-19 ndani ya UAE. Hii ilifuatiwa na kampeni ya 'Milo Milioni 100' mwaka 2021, kampeni kubwa zaidi ya kikanda ya usaidizi wa chakula iliyohusisha nchi 20 za Kiarabu, Afrika na Asia. 'Milo Bilioni Moja' ya mwaka jana ilikuwa kubwa zaidi ya aina yake kikanda, ikitoa milo bilioni 1 katika nchi 50.

4130018

captcha