IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Tuzo ya 26 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai: washindi watunukiwa (+Picha)

15:49 - April 06, 2023
Habari ID: 3476821
TEHRAN (IQNA) – Washindi watatu bora wa Tuzo ya 26 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Dubai waliarifishwa katika hafla iliyofanyika Dubai Jumanne usiku.

Zawadi ya juu ilienda kwa Saleh Ahmed kutoka Bangladesh akifuatiwa na Abbas Hadi Omar wa Ethiopia na kisha Khaled Al Burkani wa Saudi Arabia.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na washiriki wa shindano hilo pamoja na maafisa kadhaa wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Dk. Ahmed Omar Hashem, rais wa zamani wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar, pia alitunukiwa zawadi ya Shakhsia wa Kiislamu wa Mashindano ya Kimataifa ya Tuzo ya Qur'ani ya Dubai mwaka huu. Mwanawe alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya baba yake.

Wajumbe wa jopo la waamuzi pia walitunukiwa zawadi katika hafla hiyo.

Wahifadhi Qur'ani kutoka nchi 65 walishindana katika hafla hiyo ya Qur'ani ambayo ilifanyika katika kitengo cha kuhifadhi.

Jopo la waamuzi wa shindano hilo lilijumuisha wataalamu wa Qur'ani kutoka nchi mwenyeji pamoja na Saudi Arabia, Morocco, Misri, Pakistan na Bangladesh.

Tuzo la Kimataifa la Qur'ani Tukufu la Dubai (DIHQA) huandaliwa kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

 

3483070
captcha