IQNA

Uislamu

Kocha wa Kandanda wa Ureno José Morais asilimu nchini Iran

10:56 - April 27, 2024
Habari ID: 3478739
IQNA - José Manuel Ferreira de Morais, kocha wa Ureno wa timu ya Sepahan SC ya Iran, amethibitisha kwamba amesilimu.

Alitoa tangazo hilo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa baada ya moja ya mechi za Sepahan.

Ripota mmoja alimuuliza Morais kuhusu uvumi kuhusu kusilimu kwake. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 alisema, "Ndio,  nilibadilika kwa heshima ... tayari."

Wakati huo huo, tovuti ya habari za michezo ya Varzesh3 ilitoa maelezo zaidi kuhusu uamuzi wa mkufunzi huyo kukumbatia Uislamu katika maisha yake. Kulingana na ripoti hiyo, Morais aliwasiliana na wasimamizi wa klabu hiyo, akieleza nia yake katika kusilimu na  kuwaomba msaada katika mchakato wa kukumbatia Uislamu maishani.

Idara ya kitamaduni ya klabu hiyo ilitoa ushauri kwa kocha huyo na hatimaye akatamka Shahada mbili mbele ya mwanazuoni wa Kiislamu  ambapo baada ya kusilimu alisema atafuata muongozo wa madhehebu ya Kiislamu ya Shia, ripoti hiyo ilisema.

Morais alianza kazi yake ya ukocha mwaka 1999 akiwa na Benfica B. Amesimamia zaidi ya vilabu kumi katika kipindi cha miaka 25 iliyopita duniani kote. Pia amewahi kuwa kocha msaidizi katika timu za juu za Ulaya kama vile Inter Milan na Real Madrid.

Uislamu ndio dini inayokuwa kwa kasi zaidi duniani, huku idadi ya Waislamu ikitarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya mara mbili ya idadi ya watu duniani kote kati ya 2015 na 2060, kulingana na utafiti wa Kituo cha Utafiti cha Pew.

3488094

captcha