Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, gazeti la Saudi Arabia la Al Riyadh limeandika kuwa ujumbe huo wa rambi rambi umepokewa na Waziri wa Afya wa Iran Sayyid Hassan Hashimi alipokutana na mwenzake wa Saudi Arabia Khalid bin Abdulaziz Al-Falih mjini Jeddah. Katika kikao hicho mawaziri hao wawili walijadili maafa ya Mina na hali ya waliojeruhiwa waliolazwa katika hospitali za Saudia.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Khalid bin Abdulaziz Al-Falih aliwasilisha salamu za rambi rambi za mfalme wa Saudi Arbaia kwa serikali ya Iran na familia za waliopoteza maisha katika maafa ya mina na kusema ufalme huo uko tayari kushirikiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Gazeti hilo la Saudia limeandika kuwa waziri wa afya wa Iran amemshukuru mwenzake wa Saudia kwa kuandaa kikao hicho na ametaka majeruhi wa Iran wapewe huduma zinazofaa za kitiba. Aidha pande mbili ziliafikiana kuhusu kuharakishwa kutambuliwa na kukabidhiwa Iran viwiliwili vya Mahujaji wote Wairani walipoteza maisha kwa ajili ya mazishi.../mh