IQNA

Rais Hassan Rouhani

Lazima maafa ya Mina yachunguzwe

17:49 - October 03, 2015
Habari ID: 3377977
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, lazima ukweli wa maafa ya Mina, Saudia ubainishwe kupitia tume ya uchunguzi itakayosimamiwa na nchi za Kiislamu.

Rais Rouhani ameyasema hayo asubuhi ya leo mjini Tehran kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mehrabad, wakati wa kutoa heshima kwa wahanga wa maafa hayo ya Mina ambapo sanjari na kusisitiza juu ya ulazima wa kuchunguzwa kadhia hiyo, amesema kuwa, ikiwa itabainika kuwa maafisa wa Saudi Arabia walihusika kwa njia yoyote ile katika tukio hilo chungu, basi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitalinyamazia kimya. Ameongeza kuwa, Iran imetumia lugha ya busara na udiplomasia katika suala hilo, huku akisisitiza kuwa ikihitajika basi Iran itatumia lugha ya nguvu kuhusu kadhia hiyo. Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameweka wazi kwamba, ni lazima ukweli wa maafa hayo ya Septemba 24 ufahamike na kutoa shukurani za dhati kwa Wizara ya Afya, Taasisi ya Hijja na Ziara, Taasisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu inayoshughulikia masuala ya Hija, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Ndani viongozi wa bunge na hususan Kiongozi Muadhamu Ayatullahil-Udhma Sayyid Ali Khamenei, ambao nao wametaka kuchunguzwa maafa hayo.../mh

3377499

Kishikizo: rouhani mina kiislamu hija
captcha