IQNA

Wanawake Waislamu duniani wataka uchunguzi kuhusu maafa ya Mina

20:41 - October 13, 2015
Habari ID: 3385195
Umoja wa Wanawake Waislamu Duniani wametoa taarifa ya rambirambi kufuatia kuuawa maelfu ya mahujaji kutoka nchi mbali mbali katika mkanyangano wa Mina karibu na mji mtakatifu wa Makka.

Umoja huo pia umetoa wito kwa taasisi za kimataifa kufuatilia kwa karibu maafa hayo na kuzisaidia nchi ambazo mahujaji wao walipoteza maisha katika tukio hilo chungu.
Mnamo Septemba 24, mahujaji takribani 5,000 walipoteza maisha katika msongamano mkubwa uliojiri katika ibada ya Hija huko Mina wakati wa amali ya Ramy al-Jamarat ya kumpiga mawe shetani.
Tukio hilo lilijiri wiki mbili baada ya mahujaji wengine zaidi ya 100 kupoteza maisha baada ya kreni au winchi kuanguka katika Masjidul Haram mjini Makka.
Waislamu kote duniani wameukosoa vikali utawala wa Saudi Arabia kwa kushindwa kulinda usalama wa mamilioni ya Waislamu ambao hutembelea mji mtakatifu kila mwaka kwa ajili ya Hija na Umrah. Utawala wa Saudi Arabia umeonyesha kiburi kikubwa na kukataa kusikiliza malalamiko na hata mapendekezo ya Waislamu na nchi za Kiislamu kuhusu kuboresha usimamizi wa ibada ya Hija.../

3384597

captcha