IQNA

Rais Rouhani ataka mahujaji wadhaminiwe usalama

11:46 - October 14, 2015
Habari ID: 3385427
Rais Hassan Rouhani wa Iran amesisitiza umuhimu wa kudhaminiwa usalama wa mahujaji katika ibada ya kila mwaka ya Hija.

Akizungumza kwa njia ya moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa Jumanne usiku, Rais Rouhani kwa mara nyingine ametoa salamu zake za rambi rambi kufuatia maafa yaliyojiri huko Mina katika ibada ya Hija mwaka huu. Amesema Waislamu wanafaa kuhakikishiwa usalama wao wanapokwenda kutekeleza ibada hiyo tukufu na kwamba uchunguzi huo utabaini mapungufu yaliyokuwepo ili tukio hilo chungu lisijikariri katika misimu ijayo ya Hijja.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kina kubaini kiini cha maafa ya Mina.
Rais Hassan Rouhani amesema sababu zilizopelekea kutokea maafa hayo, ambapo maelfu ya watu walipoteza maisha kwenye mkanyagano walipokuwa wakitekeleza ibada ya hijja, zinafaa kuwekwa wazi kwa Iran na kwa Waislamu wote kote ulimwenguni.
Maafa ya Mina yalitokea tarehe 24 Septemba, siku ya sikukuu ya Idul Adh'ha kwenye ibada ya kumpiga mawe shetani, maarufu kama Jamarat.
Mamlaka za Saudi Arabia zinalaumiwa kwa kutosimamia vizuri amali hiyo na kupelekea kutokea maafa hayo makubwa.../mh

3385203

captcha