IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Magaidi hawana uhusiano na Uislamu, Wanapinga Maulidi

18:20 - December 25, 2016
1
Habari ID: 3470759
IQNA-Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah amesema magaidi wakufurishaji wanaotenda jina magharibi mwa Asia na Afrika hawana uhusiano wowote na Uislamu wala Matume Mtukufu Muhammad SAW.

Sayyid Hassan Nasrallah amesema hayo Ijumaa kusini mwa Beirut mji mkuu wa Lebanon na kubainisha kwamba idiolojia inayotumiwa na magaidi hao wenye misimamo mikali chimbuko lake ni Uwahhabi. Ameongeza kuwa Mawahhabi wamepuuza masuala muhimu ya Waislamu hasa kadhia ya Palestina.

Katika hotuba yake hiyo Sayyed Hassan Nasrallah amewapongeza Waislamu kwa munasaba wa Maulidi ya Bwana Mtume SAW na pia amewapongeza Wakristo kwa munasaba wa maadhimisho ya Kuzaliwa Nabii Issa AS yaani Krismasi. Kiongozi wa Hizbullah ameashiria jinai zinazotkelezwa na magaidi wakufurishaji wa Kiwahhabi na kusema fikra za Kiwahhabi ni hatari na kuongeza kuwa, "Mawahhabi wameharamisha sherehe za Maulidi ya Mtume Mtukufu Muhammad SAW na wanawalenga wanaodahimsiha Maulidi."

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi vikitaja jina la ISIS au Daesh hutumia maneno kama "Dola la Kiislamu", "Uislamu wa Misimamo Mikali", "Kundi Lenye Misimamo Mikali ya Kiislamu", "Ugaidi wa Kiislamu" na kadhalika, hatua ambayo inaonyesha kuwa, propaganda hizo ni sehemu ya njama dhidi ya Uislamu.

Ameongeza kuwa, kipindi cha miaka kadhaa iliyopita ya historia yake, katu dini ya Kiislamu haijawahi kukabiliwa na njama na hujuma za kuitia dosari dini hii tukufu kama ilivyosasa.

Sayyid Nasrallahamesisitiza kwamba, Waislamu wote wana jukumu la kidini, kihistoria na kimaadili katika mazingira haya. Kuna ulazima kwa Waislamu kutumia kila mbinu kulaani hujuma na hatua za matakfiri na kutangaza kwamba, vitendo na hatua za matakfiri hao havina uhusiano wowote na Uislamu.

Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ni kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel umekwama katika kufikia malengo ya siasa zake zilizo dhidi ya Uislamu, nchi za Kiislamuna eneo la Mashariki ya Kati kutokana na kuweko umoja baina ya matabaka mbalimbali ya wananchi na kwamba, harakati ya kitakfiri nayo haitafikia popote.

3555959

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Twaha Mruma
0
0
Natangulia kusema kwamba mimi sio msomi wala mjuzi wa Uislam. Lakini najaribu kujenga hoja.

Kwa nini tunasema magaidi hawana uhusiano na Uislam.. Ni kwa sababu tu wanapinga Maulid? ... Nguzo za Uislam na za imani hazitaji Maulid ... Kama wanamtambua Allah SW na Mtume SAW basi ni Waislam... Nawaza tu.
captcha