Shule hiyo katika mji mkuu wa Uingereza sasa inakabliwa na mashinikizo kutokana na hatua hiyo ya kuwanyima wanafunzi Waislamu haki ya kusali Sala ya Ijumaa.
Wanafunzi hao Waislamu wanasema walilazimika kusali nje baada ya shule kuwanyima idhini ya ksali ndani ya moja ya vyumba vya darasa.
Shule ya Park High imetoa taarifa na kukanusha kuwa imewazuia wanafunzi kusali Sala ya Ijumaa lakini haikutoa maelezo kuhusu sababu ambayo ilipelekea wasali katika uwanja wa shule hiyo.
Imedokezwa kuwa tatizo kama hilo liko katika shule nyingi nchini Uingereza ambapo wanafunzi Waislamu wanabaguliwa na kunyimwa idhini ya kusali Sala ya Ijumaa.