IQNA

Waislamu Ulaya

Rufaa kuhusu marufuku ya nyama Halal na Kosher Ubelgiji imekatiliwa

17:21 - February 14, 2024
Habari ID: 3478349
IQNA - Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu ilikataa rufaa dhidi ya sheria nchini Ubelgiji zinazopiga marufuku nyama ya Halal na Kosher.

Kundi la Waislamu na Wayahudi walishindwa katika kesi ya mahakama nchini Ubelgiji kuhusu sheria za haki za wanyama zinazowazuia kuchinja kwa mujibu wa kanuni za Halal za Kiisalmu na na Kosher za Kiyahudi.

Marufuku ya kuchinja bila kupiga mnyama risasi ya kumlemeza kwanza ilipingwa na wawakilishi wa jamii za Waislamu wa Ubelgiji, pamoja na Wayahudi.

Waislamu na Wayahudi wamesema  sheria zilifanya iwe "ngumu, kuchinja wanyama kwa mujibu wa kanuni za dini yao".

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu ilikubali sheria hizo za Ubelgiji, zilizopitishwa kando katika maeneo ya watu wanaozungumza Kiholanzi na Kifaransa nchini Ubelgiji.

Sheria ya Ulaya inaruhusu uhuru wa kidini kuzuiwa kwa kisingizio cha "maadili ya umma" - na hii iinahusu pia  wanyama, mahakama iliamua.

Jopo la majaji saba pia lilikataa madai ya waombaji kwamba itakuwa "vigumu, ikiwa haiwezekani, kupata nyama kulingana na imani yao ya kidini".

Serikali ilisema watu bado wanaweza kununua nyama wanayopendelea kutoka nje ya nchi, au kutoka Brussels, ambayo haijapitisha sheria kali kama hiyo.

Vikundi vya Waislamu na Wayahudi "havikuwa vimeonyesha kuwa upatikanaji wa nyama kama hiyo umekuwa mgumu zaidi," mahakama ilisema. Madai kwamba sheria hizo zilikuwa za kibaguzi pia zilishindikana.

Majaji katika Mahakama ya Haki ya Umoja wa Ulaya, mahakama tofauti, hapo awali walikuwa wameunga mkono mamlaka ya Ubelgiji katika uamuzi wa 2020.

3487186

Kishikizo: ubelgiji waislamu halal
captcha