Hujjatul Islam Seyed Abdol Fattah Navab, mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Masuala ya Hija na Ziyara na Ayatullah Mohsen Qomi, mkuu wa masuala ya kimataifa katika Ofisi ya Kiongozi Muadhamu ni miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho.
Kituo cha Utafiti wa Hija na Ziyara kimeandaa mkutano huo kwa ushirikiano na taasisi na vituo vingine 30 kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuharibiwa kwa makaburi ya Baqi mjini Madina.
Vitabu kumi na tano vilivyoandikwa kuhusu makaburi ya Baqi na waliozikwa humo pia vilizinduliwa wakati wa sherehe za ufunguzi.
Mkutano huo umehudhuriwa na wanazuoni, wanafikra na watafiti wa vyuo vikuu na seminari kutoka katika ulimwengu wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa waandaaji, makala 66 ziliwasilishwa katika sekretarieti ya mkutano huo.
Washiriki katika tukio la siku mbili la kitaaluma wamejadili mada kama vile masomo ya kisiasa na kijamii kuhusu Baqi, tafiti za kisasa kuhusu Baqi, masomo ya kihistoria na ustaarabu wa Baqi, na masomo ya kimataifa kuhusu Baqi.
Makaburi katika Jannatul Al-Baqi (Makaburi ya Baqi) yalibomolewa kabisa na Mawahabi wenye misimamo mikali mnamo tarehe 8 Shawwal katika mwaka wa 1345 AH (Aprili 21, 1925).
3487987