iqna

IQNA

mina
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, hatua yoyote ile - hata ndogo kiasi gani - ya kuwavunjia heshima mahujaji wa Iran na kutotekelezwa majukumu yanayotakiwa kuhusiana na maafa ya mahujaji waliopoteza maisha katika maafa ya Mina, itakabiliwa na jibu kali kutoka Iran.
Habari ID: 3375966    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/30

Serikali ya Indonesia imesema siku kadhaa baada ya maafa ya Mina, utawala wa Saudi Arabia umeizuia nchi yake kuwatambua au kutoa msaada wa kitiba kwa raia wake.
Habari ID: 3375825    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/30

Saudi Arabia imesema kuwa itawazika kwenye makaburi ya umati mahujaji walioaga dunia katika tukio la Mina ambao imeshindakana kutambuliwa.
Habari ID: 3374469    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/29

Wizara ya Afya ya Saudi Arabia imetangaza kuwa, idadi ya Mahujaji walipoteza maisha katika maafa ya Mina imefikia 4,173.
Habari ID: 3374468    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/29

Rais Rouhani wa Iran
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, ukosefu wa busara na tadbiri katika utawala wa Saudia ndio chanzo cha mahujaji kupoteza maisha kidhulma.
Habari ID: 3374466    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/29

Mfalme Salman wa Saudi Arabia ametoa amri ya kukusanywa kanda zote za kamera zilizosajili maafa ya kusikitisha ya Mina.
Habari ID: 3372681    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/28

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Ulimwengu wa Kiislamu una maswali mengi ya kuuliza kuhusu maafa yaliyotokea Mina nchini Saudi Arabia.
Habari ID: 3372415    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/27

Qarii mashuhuri na mtajika wa Misri, Ustadh Dkt. Abdul Fattah Tarouti ametuma salamu zake za rambi rambi kufuatia kurejea kwa Mola wao maqarii hao wawili wa kimataifa waliokuwa wakitekeleza ibada ya Hija katika eneo la Mina karibu na mji mtakatifu wa Makkah.
Habari ID: 3372198    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/27

Qarii mashuhuri wa Iran aliokuwa katika msafara wa Qur'ani wa mahujaji amethibitishwa kuaga dunia kufuatia msongamano mkubwa wa mahujaji katika eneo la Mina karibu na mji mtakatifu wa Makka.
Habari ID: 3370739    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/26

Sayyid Hassan Nasrullah
Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Saudi Arabia inalazimika kukabidhi masuala ya kusimamia na kuendesha ibada ya Hija kwa nchi za Kiislamu.
Habari ID: 3370688    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/26

Gazeti la al Diyar la Lebanon
Imearifiwa kuwa msafara wa mwanamfalme wa Saudia, Mohammad Bin Salman Aal Saud katika eneo la Mina, ndiyo sababu ya kupelekea msongamano na kufariki maelfu ya mahujaji katika eneo hilo karibu na mji mtakatifu wa Makka.
Habari ID: 3369304    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/25

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametangaza siku tato za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya mamia ya mahujaji waliokuwa katika ibada ya Hija huko Mina, karibu na mji mtakatifu wa Makka.
Habari ID: 3367103    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/24

Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu wasiopungua 1,000 wamefariki dunia na wengine 1,500 wamejeruhiwa katika msongamano wa mahujaji wakati wa kutekeleza ibada ya Hija huko Mina karibu na Makka.
Habari ID: 3367053    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/09/24