IQNA

Gaidi aliyeuhujumu Msikiti Norway afungwa jela miaka 21

22:08 - June 11, 2020
Habari ID: 3472856
TEHRAN (IQNA) – Gaidi aliyeuhujumu msikiti nchini Norway amehukumiwa kifungo cha miaka 21 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua dada yake wa kambo na kufyatua risasi ndani ya msikiti mjini Oslo, mwezi Agosti mwaka jana.

Gaidi huyo, Philip Manshaus, amesema alitekeeza jinai hiyo kutokana na misimamo yake mikali ya itikadi za wazungu wa mrengo wa kulia wanaopinga kuwepo wahajiri na Waislamu katika nchi hiyo ya Ulaya. Wakali wa gaidi huyo awali alitaka atambuliwe kuwa ni mwendawazimu lakini mahakama imebaini kuwa alikuwa na akili timamu na hivyo amehukumiw akifungo hicho ambacho kinaweza kuongezwa iwapo ataonekana badi ni hatari kwa jamii.

Manshaus, 22, alikiri kumuua dada yake wa kambo, Johanne Zhangjia Ihle-Hanse, mwenye asili ya China, na kushamblia Kituo cha Kiislamu cha al-Noor katika eneo la Baerum, katika mji mkuu wa Norway, Oslo.

Manshaus amesisitiza mahakamani kuwa vitendo vyake si jinai na kwamba kile kinachomsikitisha sana ni kuwa hakuweza kuwadhuru watu wengi. Amedai kuwa vitendo vyake si ugaidi na kwamba alikuwa anawalinda wazungu wenyeji wa Ulaya.

3471667

Kishikizo: norway waislamu msikiti
captcha