IQNA

Tarjama ya Kiganda ya Dua Tawwasul

21:39 - July 23, 2014
Habari ID: 1432795
Kwa mara ya kwanza, Dua Tawwasul imetarjumiwa na kuchapishwa kwa lugha ya Kiganda nchini Uganda.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA  Afrika Mashariki,  dua hiyo imetarjumiwa kwa hisani ya Idara ya Utamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Uganda. Mtarjumi wa Dua Tawwasul kwa Kiganda (Luganda) ni Musa Muganza Sowedi mtarjumi mashuhuri ambaye anafahamu vizuri lugha tatu za Kiarabu, Kiingereza na Kiganda  ambapo amechukua miezi sita kukamilisha kazi hiyo.
Nakala elfu mbili za tarjama kamili za Dua Tawassul na Dua Kumayl kwa lugha ya Kiganda zimetayarishwa na kusambazwa kote Uganda katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Sheikh Musa Sowedi amesomea masomo ya Kiislamu katika vyuo vya kidini huko Jinja  Uganda na pia nchini Kenya. Yeye ni kati ya wanaharakati mashuhuri wa Kiislamu na utamaduni na pia ana Shahada ya Kwanza lLugha ya Kiingereza kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda.

1431903

captcha