IQNA- Katika dunia ya leo yenye pilika pilika nyingi na mwendo wa haraka, wakati mwingine tunahitaji kusimama kwa muda mfupi na kupata utulivu. Mfululizo wa "Sauti ya Wahyi" kwa kuchagua baadhi ya aya kwenye Qur'ani Tukufu na sauti ya kupendeza ya Ustadh Behrouz Razawi, ni mwaliko wa safari ya kiroho na yenye kuinua roho. Mfululizo huu mfupi lakini wenye maudhui ya kina, unawaletea nyakati za utulivu na matumaini.
IQNA – Hafla ya uzinduzi wa Maonesho ya Sanaa za Qur’an ya Duha, yaliyoandaliwa na Shirika la Qur’an la Wasomi wa Iran, ilifanyika jioni ya Jumapili, Novemba 16, 2025, katika Makumbusho ya Sanaa za Kidini ya Imam Ali (AS), mjini Tehran.
IQNA – Hafla ya kufunga Tamasha la 39 la Kitaifa la Qur’ani na Etrat kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Iran ilifanyika Jumapili, tarehe 9 Novemba 2025, katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Azad, tawi la Isfahan.
IQNA – Katika mandhari ya vijijini vya Malawi, taswira za watoto wakishiriki kwa ari katika miduara ya kisomo cha Qur'ani Tukufu zimeanza kuvutia mitandaoni, zikidhihirisha mchango hai wa jamii ya Waislamu wachache nchini humo.