IQNA

Mjumuiko mkubwa wa watu Tehran kulaani jinai za utawala wa Israel huko Ghaza

12:00 - May 20, 2021
Habari ID: 3473929
TEHRAN (IQNA)- Maandamano yamefanyika mjini Tehran kulaani jinai zinazoendelea kufanywa na utawala katili wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia katika Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa taarifa, maandamano hayo yamefanyika katika Medani ya Imam Hussein AS mjini Tehran ambapo washiriki kutoka matabaka mbalimbali walikuwa wamebeba bendera za Palestina ili kueleza mfungamana wao na taifa hilo linalokandamizwa. Waandamanaji hao pia walisikika wakitoa nara kama: "Mauti kwa Marekani", "Mauti kwa Israel", kama njia ya kueleza hasira zao kwa jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Mijumuiko kama hiyo imefanyika pia katika miji mingine ya Iran kuwaunga mkono Wapalestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran (IRGC) Meja Jenerali Hossein Salami  amehutubu katika mjumuiko huo na kusema Iran itaendelea kuunga mkono taifa la Palestina.

 Salami amepongeza mapambano shupavu ya Wapalestina mkabala wa hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema zaidi ya thuluthi mbili ya miji ya utawala wa Kizayuni imeshambuliwa kwa maroketi ya Wapalestina kutoka Ghaza na hivyo Wazayuni hawakuwa na pa kukimbilia.  Amesema ngao ya makombora ya utawala wa Kizayuni wa Israel imeshindwa kukabiliana na maelfu ya makombora ya Wapalestina.

Kamanda Mkuu wa IRGC amesema Waisraeli wamekerwa sana na mwamko mkubwa katika harakati za mapambano ya Palestina. Aidha amesema kushindwa Israel ni alama ya kushindwa Marekani na kuongeza kuwa, leo hadhia ya Palestina ni kadhia ya dunia nzima. Amesema Wamarekani na Waisraeli wanakabiliwa na hali ngumu kwani iwapo watasitisha vita Ghaza watakuwa wamefeli na iwapo wataendeleza vita watapata pigo.

 
 

3474771

Kishikizo: palestina ghaza iran israel
captcha