Kaimu Katibu Mkuu wa Shirika la Wakfu la Kuwait Mansour Al Saqabi amesema lengo la mashindano hayo ni kuwahimiza vijana wa Kuwait kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu na watakaofanya vizuri katika mashindano hayo wataiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.
Al Saqabi amesema nara na kauli mbiu ya mashindano hayo mwaka huu ni اِطْمَئِنَّ (iṭmaʾinna) na yanafanyika chini ya usimamizi wa Emir wa Kuwait Sheikh Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah ambaye ni kiongozi wa nchi hiyo ya Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi.
Ameongeza kuwa baada ya kufanyika mashindano ya mchujo katika maeneo mbali mbali ya nchi fainali zifafanyika katika Msikiti wa Jamia wa Kuwati mwezi Oktoba kwa muda wa wiki mbili na washindi watatangazwa.