Mabango hayo yamewekwa katika wakati huu wa mkesha wa kukumbuka kuuawa shahidi Kamanda Soleimani na wanajihadi wenzake.
Muhammad al Buraim, mkurugenzi wa habari katika Kamati za Muqawama za Wananchi wa Palestina amesema Wapalestina wanachukua fursa ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Qassem Soleimani kutangaza kuwa wataendeleza harakati za za muqawama au mapambano .
Amesema harakati za mapambano ya ukombozi wa Palestina zitaendeleza nji ya ukombozi wa Quds ambayo ni njia iliyokuwa ikifuatwa na Shahidi Soleimani.
Al Buraim ameongeza kuwa Palestina kati haitasahau damu ya Shahidi Soleimani ambayo alijitolea katika kuunga mkono taifa la Palestina.
Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.