IQNA

Ibada ya Hija

Operesheni ya kuosha na kusafisha Ka’aba Tukufu

19:28 - June 04, 2022
Habari ID: 3475335
TEHRAN (IQNA)- Operesheni ya kuosha na kusafisha Ka’aba Tukufu huko Makka imekamilika ili kuandaa mahali patakatifu kwa ajili ya Hija ijayo.

Idara ya Mkuu wa Msikiti Mkuu na Misitikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina imesema timu maalumu ilitumia teknolojia ya hivi kisasa kabisa ya kusafisha kufanya operesheni ya mara kwa mara ya kuosha ukuta wa Ka'aba Tukufu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Muhammad bin Muslih al-Jaberi, afisa mwandamizi wa idara hiyo, timu kwanza iliondoa vumbi kutoka sehemu zote za kuta za Ka’aba, ambapo mbali na kuta maeneo mengine yaliyosafishwa ni paa na mlango. Kwanza maji ya kawaida yametumika kuosha eneo hilo takatifu na baada ya kukauka, Ka’aba  ilioshwa tena kwa maji ya waridi.

Utumiaji wa mbinu na teknolojia mpya umesaidia kuharakisha kazi ya kusafisha na kupunguza gharama, afisa huyo alisema.

Matayarisha ya Ibada ya Hija yamekamilika na Mahujaji wanatazamiwa kuanza kuingia katika mji mtakatifu wa Mecca wiki ijayo.

Saudi Arabia imetangaza kuwa itapokea mahujaji wa kigeni kwa ajili ya Hija mwaka huu baada ya miaka miwili ya kusimamishwa kazi kutokana na janga la COVID-19.

3479167

captcha