IQNA

Teknolojia

Roboti zatumika ksambaza Misahafu kwa Mahujaji katika Msikiti Mkuu wa Makka

17:56 - July 12, 2022
Habari ID: 3475493
TEHRAN (IQNA) – Huduma mpya ya kisasa imezinduliwa katika Msikiti Mkuu wa Makka, Masjid al-Haram, mwaka huu ili kusambaza Misahafu kwa waumini na Mahujaji.

Roboti imetumika kusambaza nakala za Quran huku mahujaji wakimaliza safari yao ya Hajj huko Makka.

Akitoa maelezo juu ya kifaa hicho, Naibu Katibu Mkuu wa Rais wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina Badr bin Abdullah Al-Firaih alisema roboti hiyo ambayo hupita kwa urahisi katikati ya umati wa watu, ina uzito wa kilo 59 na kasi inayoweza kudhibitiwa ya mita 1.2 - 5 kwa sekunde na uwezo wa kubeba kilo kumi.

Takriban mahujaji milioni moja kutoka nchi mbalimbali walifanya ibada ya Hija mjini Mecca mwaka huu, baada ya kufanya ibada hiyo na idadi ndogo ya mahujaji katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kutokana na janga la virusi vya corona.

3479670

captcha