IQNA

Misikiti Miwili Mitakatifu

Khutba za Sala ya Ijumaa Misikiti Mitakatifu ya Makka na Madina kutarjumiwa kwa Kichina

21:06 - December 12, 2022
Habari ID: 3476238
TEHRAN (IQNA) - Kichina kimeongezwa kwenye orodha ya lugha ambazo hutarjumiwa au hutafsiriwa katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, Al Masjid Al Haram, na Msikiti wa Mtume SAW, Al-Masjid an-Nabawi, katika Vyombo vya Habari.

Uongozi  Mkuu wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu ulitangaza hili, kwa mujibu wa tovuti ya Mecca News.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa tangu miaka ya nyuma umekuwa ukitekelezwa mpango ambapo hutba za sala ya Ijumaa pamoja na Khutba ya Arafa wakati wa ibada ya Hija hutarjumiwa kwa lugha tofauti.

Kwa kujumuishwa kwa Kichina, idadi ya lugha hizo imefikia 14, ofisi ya Uongozi  Mkuu wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu umebaini.

Kiingereza, Kifaransa, Kimalayu, Kiurdu, Kiajemi, Kirusi, Kibengali, Kituruki, Kihausa, Kihispania, Kiswahili, Kitamil na Kihindi ndizo lugha nyinginezo.

Uongozi  Mkuu wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu pia umesema kuwa umewekeza katika nyanja za akili yam ashine (AI) na maendeleo ya kidijitali, na kutoa fursa ya kutumia roboti kutoa tafsiri kwa waumini na mahujaji.

Taarifa hiyo ilisema kwamba watu wapatao milioni 200 katika sehemu mbalimbali za dunia walisikiliza Hotuba ya Arafah katika lugha 14 katika ibada iliyopita ya Hijha, kwa kutumia huduma za tafsiri za Uongozi  Mkuu wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu.

 Kuongezwa kwa Wachina katika orodha ya lugha za misikiti hiyo miwili mitakatifu kunakuja kufuatia ziara ya Rais wa China Xi Jinping nchini Saudi Arabia mapema wiki hii.

4106104

captcha