Yeni Shafaq, mtalii wa Morocco aliyesambaza video hii ameambatanisha maandishi yasemayo: "Wakati wa safari yangu katika nchi moja ya Afrika, nilikuwa nikipita kwenye kijiji kimoja kidogo na nikasikia sauti nzuri wakati wa usiku, nikaenda kuitafuta na baada ya muda niliona watoto wakiwa wanasoma aya za Quran Tukufu. Katika video iliyosambazwa, watoto hao wanasikika wakisoma Sura Maryam aya ya 30-34.
(Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai, Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai. Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.
4202312