IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Kitengo cha Kimataifa Cha Maonyesho ya 31 ya Qur'ani Tehram chamalizika

15:12 - March 29, 2024
Habari ID: 3478599
IQNA – Kitengo cha Kimataifa cha Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran kimefika ukingoni Alhamisi

Kitengo hiki kilishuhudia ushiriki kutoka mataifa mbalimbali. Nchi zenye Waislamu wengi kama vile Umoja wa Falme za Kiarabu, Algeria, Saudi Arabia, Tunisia, Kuwait, Thailand, Bangladesh, Iraq, Palestina, Malaysia, Indonesia, Sri Lanka, India, Bahrain na Pakistan zilihudhuria.

Mbali na hayo, nchi zisizo za Kiislamu kama Ufaransa, Uchina, Kroatia, na Urusi pia zilishiriki kikamilifu. Wawakilishi kutoka nchi nyingine saba walipamba maonyesho hayo wakiwa wageni.

Katika muda wa siku nane, vikao vya kila siku v

ilifanyika katika sehemu ya kimataifa, na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi zilizoshiriki.

Onyesho la hadhara la vipande vya sanaa kutoka nchi mbalimbali lilikuwa kivutio kingine cha maonyesho hayo.

Kipengele muhimu cha maonyesho ya mwaka huu kilikuwa uwekaji wa sehemu ya kimataifa moja kwa moja kwenye mlango, na kuimarisha mwonekano wake na ufikiaji.

Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yalianza tarehe 20 Machi Mosalla mjini Tehran. Maonyesho hayo, huanza kila  siku saa kumi na moja jioni hadi saa sita usiku na yataendelea hadi Aprili 2.

Maonyesho hayo yanajulikana kwa mazingira yake ya kifamilia, yakihudumia wageni wa rika zote. Aidha katika maonyesho hayo kuna taasisi mbalimbali za Qur'ani na mashirika ya serikali. Pia mwaka huu yametilia mkazo masuala ya Gaza na Palestina na nafasi ya Qur'ani katika kukuza muqawama.

Madhumuni ya maonyesho hayo ni kufahamisha watu kuhusu fikra za Qur'ani kupitia njia za kisanii, kitamaduni na yamelenga zaidi watoto na vijana.

3487739

Habari zinazohusiana
captcha