IQNA

Kamanda wa Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mapambano yataendelea hadi Quds ikombolewe

0:30 - January 22, 2015
Habari ID: 2743221
Kamanda wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC amesema mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni yataendelea hadi Quds Tukufu ikombolewe.

Meja Jenerali Mohammad Ali Jafari ameyasema hayo leo Jumanne katika mazishi ya afisa wa IRGC Shahidi Brigedia Jenerali Mohammad Ali Allahdadi aliyeuawa hivi karibuni katika hujuma ya utawala wa Kizayuni katika eneo la Quneitra nchini Syria. Meja Jenerali Jafari amesema orodha ya waliouawa shahidi katika eneo la Quneitra ni ishara ya umoja wa umma wa Kiislamu. Ameongeza kuwa Shahidi Allahdadi daima alikuwa na moyo wa aina yake wa kujitolea muhanga. Amesisitiza kuwa ujumbe wa kuuawa shahidi jenerali huyo Muirani ni kuwa; mapambano yataendelea hadi Quds itakapokombolewa.

Ikumbukwe kuwa siku ya Jumapili, Helikopta mbili za utawala wa Kizayuni zilishambulia kikosi cha kulinda doria cha wanamapambano wa Hizbullah katika eneo la Quneitra, karibu na laini inayotenganisha eneo la Syria la Milima ya Golan na upande unaokaliwa kwa mabavu na Israel. Katika shambulizi hilo la kigaidi watu saba waliuawa shahidi akiwemo Jihad Mughniya mwana wa Shahidi Imad Mughniya ambaye pia aliuawa katika hujuma ya kigaidi ya Israel. Viongozi wa kijeshi wa Iran na pia viongozi wa Hizbullah wamesisitiza kuwa kufuatia ugaidi huo wa kiserikali, adui Muisraeli atajibiwa kwa pigo kali wakati muafaka.

2739954

captcha