IQNA

Wanajeshi wa Utawala wa Kizayuni wamuua shahidi kijana Mpalestina Quds Tukufu

10:51 - September 05, 2016
Habari ID: 3470549
Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameshambulia kambi ya wakimbizi wa Kipalestina katika Quds Tukufu (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu na kumuua shahidi kijana Mpalestina.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA,  wanajeshi katili wa Israel waliwafyatulia risasi vijana wawili Wapalestina katika kambi ya wakimbizi ya Shu’fat na kumuua shahidi kijana Mpalestina na kumjeruhi mwingine.

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamedai kuwa, eti vijana hao walikuwa wanakusudia kuwakanyaga askari Waisraeli kwa gari na hivyo wakafyatuliwa risasi.

Wakaazi wa eneo hilo wamemtambua kijana aliyeuawa shahidi kuwa Mustafa Nimr kutoka mtaa wa Dahieh al-Salam mjini Anata yapata kilomita nne kaskakzini mashariki mwa Quds Tukufu.

Maeneo mbalimbali ya Palestina yamekuwa yakishuhudia mapambano makali tokea Oktoba mwaka 2015 ambapo Wapalestina wanalalamikia ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel na njama za kuuyahudisha mji wa Quds na kuharibu Msikiti wa Al Aqsa ambao ni qibla cha kwanza cha Waislamu.

Aidha takribani Wapalestina 7000 wanashikiliwa katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kufuatia ukatili wa wanajeshi wa Israel, tokea wakati huo hadi sasa Wapalestina zaidi ya 235 wameuawa shahidi.

3527894

captcha