Vita vya siku 11 vilivyomalizika jana usiku, vilianza baada ya utawala wa Kizayuni kuvamia na kuharibu nyumba za wakazi wa eneo la Sheikh Jarrah huko Baitulmuqaddas Mashariki na vile vile kukivunjia heshima Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa.
Wananchi wa maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina walimiminika mitaani na barabarani kushangiria ushindi, sekunde chache baada ya kutangazwa kuanza utekelezaji wa kusimamishwa vita baina ya utawala wa Kizayuni wa Israel na wanamuqawama wa Palestina, saa nane kamili usiku kwa majira ya eneo hilo.
Utawala vamizi wa Kizayuni wa Israel, jana saa nane usiku utawala huo ulianza kutekeleza usimamishaji vita kwa kuhofia vipigo zaidi vya makombora na maroketi ya wanamapambano wa Palestina.