IQNA

Khatibu wa Sala Ijumma Tehran: Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran ni mapinduzi ya kihistoria

17:03 - February 11, 2022
Habari ID: 3474917
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu yameleta matumaini kwa wanyonge na wapigania ukombozi wa mataifa yao kama ambavyo yametia nguvu masuala ya kiroho na kimaanawi ulimwenguni.

Hujjatul Islam Mohammad Javad Haj Ali Akbari amesema hayo katika khutba za leo za Sala ya Ijumaa hapa Tehran na kuongeza kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran ni mapinduzi ya kihistoria ambayo hivi sasa yako kwenye kipindi muhimu sana.

Akiashiria maadhimisho ya mwaka wa 43  ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kufikia kileleni leo sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu ambayo yaliliweka taifa la Iran kwenye njia iliyonyooka amesisitiza kuwa, mapinduzi haya matukufu yameleta matumaini na moyo mpya kwa wanyonge na wapigania ukombozi wa mataifa yao kama ambavyo yametia nguvu pia masuala ya kimaanawi na kiroho katika kona zote za dunia kiasi kwamba leo hii mataifa yaliyokuwa yamenyongeshwa yamepata nguvu za kupigania ukombozi wao. Amesema: Wakati huo huo lakini Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran ni jinamizi kwa madola ya kiistikbari ya kibeberu kutokana na kusimama kwake imara kupambana na dhulma.

Hujjatul Islam Mohammad Javad Haj Ali Akbari pia amesema, nyota ya Mapinduzi ya Kiislamu inameremeta kwa subira na shukrani kwa Allah na italifikisha taifa la Iran katika zama za kudhihiri Imam Mahdi AS na kufanikisha matarajio na malengo yote matukufu ya taifa hili.

Vile vile amesema, "Jihadi ya Kubainisha Ukweli" ni jambo la wajibu kwa kila mtu katika taifa hili na kwamba matabaka yote ya wananchi wanapaswa kupambana vilivyo na njama zote za adui za kupotosha ukweli wa mambo.

4035609

captcha