IQNA

Algeria yakosoa ubaguzi dhidi ya mchezaji kandanda Muislamu nchini Ufaransa

23:24 - February 23, 2022
Habari ID: 3474967
TEHRAN (IQNA)- Shirikisho la Soka la Algeria limelaani shambulizi la kibaguzi la hivi majuzi dhidi ya mwanasoka Muislamu raia wa Algeria nchini Ufaransa.

Mashabiki wa Ufaransa wameripotiwa kuendesha mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya Mohamed Youcef Belaïli, winga wa Brest, katika mechi dhidi ya Reims siku ya Jumapili.

Ikilaani mashambulizi hayo, shirikisho hilo lilionyesha uungaji mkono wake kamili kwa Belaïli.

Tabia hii ya kishenzi ni tofauti na roho ya mchezo wa haki, lilibaini shirikisho hilo.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 1-1 na mashambulizi ya maneno yaliiibuka baada ya Belaïli kukosa penalti katika dakika ya 53. "Hii ni Ufaransa, rudi nchini kwako" iliripotiwa kuwa moja ya nyimbo za kibaguzi.

Katika taarifa baada ya mechi hiyo, Brest alitangaza kwamba uchunguzi wa madai hayo utafunguliwa kwa ushirikiano wa Reims.

Chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu zimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni huku serikali ikionekana kufuata sera rasmi za kuwagbagua Waislamu.

4038277

captcha