Itikafu itaanza tena katika kipindi cha siku chache zijazo wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani baada ya kusimamishwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na janga la corona.
Tangazo hilo limetolewa na mkuu wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu Dkt. Abdul Rahman Sudai ambaye amesema taratibu za kufuatwa na wanaoshiriki Itikafu zitatangazwa hivi karibuni.
Kabla ya kuzuiwa kwa muda, karibu waumini laki moja walikuwa wakishriki katika Itikafu katika misikiti hiyo miwili wakati wa siku 10 za mwisho za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Hivi kairbuni pia mijumuiko mkiubwa ya futari itaruhusiwa tena katika Misikiti Miwili Mitakatifu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani baada ya kuzuiwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na janga la COVID-19.
Haya yanakuja siku chache baada ya uamuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi kuondoa kanuni zilizokuwa zinatakelezwa za kuzuia kuenea corona zikiwemo za kutokaribiana waumini Msikiti Mkuu wa Makkah, Msikiti wa Mtume SAW mjini Madina na misikiti mingine. Aidha si sharti tena waumini kuvaa barakoa.
Aidha si sharti tena kwa waumini wanaoenda Saudia kwa ajili ya Hija Ndogo au Umrah kuwa na chanjo ya corona au vipimo vya corona.