IQNA

Uislamu unaenea

Aliyekuwa mchezaji wa Kickboxing Andrew Tate athibitisha kuwa Muislamu

21:39 - October 31, 2022
Habari ID: 3476012
TEHRAN (IQNA) – Mchezaji aliyestaafi wa masumbwi aina ya kickboxing Andrew Tate amethibitisha kuwa yeye ni Muislamu baada ya klipu yake akisali katika msikiti mmoja Dubai akiwa na rafiki kuenea kwenye mitandao ya kijamii.

Alithibitisha kuwa alisilimu baada ya klipu hiyo inayomuonyesha akifundishwa Sala ya Kiislamu na Tam Khan kusambaa wiki hii.

Katika taarifa kupitia  akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii Gettr, mchezaji huyo wa zamani wa kickboxing aliandika hivi: "Hii ndiyo sababu mimi ni Mwislamu. Mkristo yeyote anayeamini katika mema na kuelewa vita ya kweli dhidi ya uovu lazima aongoke.” Alimaliza kwa kunukulu aya ya 60 ya Surat Ar Rum katika Qur’ani Tukufu isemayo:  “Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki.”

Tangazo la Andrew linakuja baada ya kuhojiwa kuhusu mawazo yake juu ya Uislamu mapema mwaka huu na kuelezea dini hiyo kama "dini ya mwisho ya kweli duniani".

Mapema wiki hii, Muislamu wa Uingereza na mpiganaji wa zamani wa MMA Tam Khan alisambaza klipu akiwa na Andrew katika msikiti huko Dubai, UAE.

Klipu hiyo, iliyoandikwa 'Alhamdhulillah' ambayo tafsiri yake ni 'Asifiwe Mungu' kwa Kiarabu, ilimuonyesha Tam akisali, huku Andrew akiiga harakati zake.

Klipu hiyo ilizua hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii na watu wengi walisema kwamba Andrew alikuwa amesilimu.

Tam amemtetea  utokana na chuki za mtandaoni zilizoenezwa dhidi yake na akasema katika chapisho la Twitter kwamba: "Mimi binafsi namjua Andrew na Mashallah mapenzi yake kwa Uislamu ni ya kweli na ni ya hakika…Yeye ni mmoja wetu..."

Kulingana na tovuti yake, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ameshindana katika uzani wa cruiserweight na uzani wa juu.

3481011

captcha