IQNA

Taazia

Khalid Abdul Basit, mwanae qarii maarufu wa wa Misri aaga dunia

22:40 - January 12, 2023
Habari ID: 3476392
TEHRAN (IQNA) – Khaled Abdul Basit Abdul Samad, mtoto wa marehemu qari maarufu wa Misri Ustadh Abdul Basit Abdul Samad alifariki siku ya Jumatatu.

Alikuwa akisumbuliwa na Kisukari kwa muda mrefu na aliugua sana katika wiki za hivi karibuni.

Khaled ameshazikwa katika kaburi la familia katika eneo la al-Basatin.

Khitma yake ilifanyika katika Msikiti wa Al-Hamidiya al-Shazliya huko Giza siku ya Jumanne, na kuhudhuriwa na wasomaji wakuu wa Qur'ani wa nchi hiyo.

Katika ujumbe wake siku ya Jumatatu, Redio ya Qur'ani ya Misri ilitoa salamu za rambirambi kwa familia ya Abdul Basit na kuomba rehema za Mwenyezi Mungu kwa Khaled.

Jumuiya ya Wasomaji na Wahifadhi wa Qur'ani ya Misri pia ilitoa ujumbe wa rambirambi kutokana na kifo cha wana wa Abdul Basit.

Ustadh Abdul Basit Abdul Samad anajulikana katika ulimwengu wa Kiislamu kama mmoja wa wasomaji wakubwa wa Qur'ani.

Yeye pia alikufa baada ya kuugua  ugonjwa wa kisukari na ini mnamo Novemba 1988.

Hizi hapa chini ni picha za Khitma ya Khaled

4113530

captcha