Ubabe wa kiitikadi na ukaidi ni mambo mawili yanayomshika mtu na kumpoteza.
Ubabe wa kiitikadi na ukaidi ulikuwa miongoni mwa sababu zilizofanya watu washindwe kukubali wito wa manabii wa Mungu.
Ubabe wa kiitikadi unamaanisha kushikamana kupita kiasi kwa jambo fulani, kama vile imani, kiasi kwamba mtu hutoa muhanga ukweli kwa ajili hulka hiyo. Ukaidi nao unamaanisha kusisitiza juu ya jambo fulani na kukataa kubadilisha maoni ya mtu ingawa ni kinyume na akili na mantiki. Wenye ukaidi wakati mwingi huwa wamashabaini ukweli uko wapo lakini kutokana na kiburi chao hukataa kukubali ukweli.
Watu waliokataa kuwafuata Mitume wa Mwenyezi Mungu wameelezwa katika Qur'ani Tukufu ifuatavyo: "Na hakika mimi kila nilipo waita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno!" (Aya ya 7 ya Surat Nuh)
Kulingana na aya hii, ushabiki wao ulikuwa mwingi kiasi kwamba walikataa hata kusikiliza ukweli achilia mbali kuukubali.
Sababu na mantiki ni mambo ambayo yanatoa mwelekeo kwa hatua za mtu. Wale wasiotii mantiki na akili na kujaribu kwenda kinyume na njia ya asili hawatashindwa tu bali pia kupoteza kila kitu walicho nacho. Ubaguzi na ukaidi ni mambo yasiyo na maana yanayompelekea mtu kupotea.
Hakuna sababu au mantiki inayoathiri tabia na mwenendo wa mtu ambaye ana ubaguzi. Anaangalia matukio jinsi anavyopenda sio jinsi yalivyo. Wanasisitiza njia yao mbaya na wanakataa kusikiliza sababu yoyote.
Qur’ani Tukufu katika aya mbalimbali inawataja watu wa aina hiyo ambao wamenaswa na ushupavu na ukaidi.