IQNA

Maadili katika Qur'ani / 9

Kupunguza mivutano kwa hulka njema

17:20 - July 03, 2023
Habari ID: 3477231
TEHRAN (IQNA) – Tangu Adam (AS) alipokuja duniani hadi Siku ya Kiyama, matatizo mengi yanayowakabili wanadamu yanaweza kutatuliwa ikiwa tutafaulu kuwa na hulka njema.

Ufunguo mdogo unaofungua kufuli kubwa ni upi hasa? Ni tabia njema na hulka njema.

Husn Khulq (hulka njema) ni msururu wa sifa zinazomfanya mtu kupendwa na watu. Husn Khulq ina matokeo mengi mazuri. Kwa mfano, husaidia mtu kuvutia upendo na huruma ya watu. Hilo litamsaidia kuvutia imani ya watu na vivyo hivyo baraka nyingi zaidi huja.

Ndiyo maana Mwenyezi Mungu anamwambia Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) ndani ya Qur'ani Tukufu kwamba: "Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio wewe (Muhammad) umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia." (Aya ya 159 ya Surah Al-Imran)

Husn Khulq pia huleta utulivu wa akili na husaidia mtu kuishi maisha marefu. Leo tunaona kwamba vifo vingi husababishwa na mfadhaiko, mahangaiko, na visababishi sawa na hivyo.

Imamu Sadiq (AS) alisema kufanya matendo mema na kuwa na Husn Khulq husaidia nyumba kustawi na kumfanya mtu aishi maisha marefu.

Wataalamu wa maadili wanapendekeza njia kadhaa za kufikia Husn Khulq. Wao ni pamoja na:

1- Kutenda kinyume na matamanio ya mtu:

Kwa njia hii, mtu anayejua, kwa mfano, kwamba ana ugonjwa unaoitwa ubahili, hutenda licha ya ubahili wake na kwa ukarimu hutoa kwa wengine alichonacho. Ama ikiwa ana husuda, humsifu na kumpongeza yule anayemwonea wivu.

2- Kufuata mfano wa kuigwa:

Mwenyezi Mungu anamsifu Mtukufu Mtume Muhammad  (SAW) kwa ajili ya Husn Khulq wake: “Umefikia kiwango cha juu cha maadili.” (Aya ya 4 ya Surah Al-Qalam)

Kwa hiyo Mtukufu Mtume (SAW) na Maimamu (AS) ni vigezo bora zaidi vya kwani Seerah na mwenendo wao vinaweza kutusaidia kukuza Husn Khulq.

captcha